BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN: HATUSHINDANI NA YANGA NA TUTAONDOKA POINTI ZOTE TATU

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kwenye mchezo wa leo dhidi ya Yanga hawatakuwa na jingine zaidi ya kuhakikisha wanapata alama zote tatu na kujiweka mbele zaidi katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuelekea mchezo huo, Sven amesema vijana wake wako tayari kila mmoja akiahidi mchezo mzuri kuhakikisha wanapata ushindi

"Tutacheza mchezo huu kama sio mchezo wa Ligi sababu kila mmoja anajua tumewaacha kwa alama kadha"

"Tutaucheza kama mchezo wa kweli na wa kipinzani kwahiyo tunajiandaa kuchukua alama tatu na kusonga mbele ili mwisho wa msimu tushinde, "
amesema Sven

Nae nahodha wa mabingwa hao wa nchi John Bocco amesema hesabu zao ni kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu



"Sisi kama wachezaji tumejiadaa vizuri kwa mchezo wa kesho. Tunaahidi kwenda kucheza mchezo wa kujituma ili tuwafurahishe mashabiki wetu na ili tuweze kupata alama zote tatu"

Simba itaingia kwenye mchezo wake ikiwa na kikosi chake kamili, Miraji na Ndemla ndio watakosekana kwa kuwa ni majeruhi

"Kwa upande wetu kila mmoja yupo fiti isipokuwa kwa Miraji na Ndemla ambao ni majeruhi. Nategemea hali nzuri kesho ambayo itaturuhusu kucheza mpira na kufurahia mchezo," amebainisha mkufunzi wa Simba, Sven

Post a Comment

0 Comments