JAMES KOTEI ATOA YA MOYONI KUHUSU MKUDEKiungo wa zamani wa Simba James Kotei amemvulia kofia mwamba Jonas Mkude akibainisha kuwa ni aina ya wachezaji ambao sio wengi duniani.Kotei amesema Mkude anastahili kuungwa mkono na kupewa sapoti ili kuhakikisha kipaji chake kinainufaisha Simba pamoja na Tanzania kwa ujumla

"Kwa maoni yangu, nina heshima kubwa kwa Mkude..Ni kipaji cha pekee na mtu muhimu kwa klabu ya Simba"

"Mtu wa aina yake ni ngumu sana kupatikana, jivunieni pia muungeni mkono. Lakini namkumbusha Mkude kuwa afahamu watu wanampenda sana, wanachotaka kutoka kwake ni manufaa ya kipaji alichonacho," 

aliandika Kotei kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.Pamoja na kuwa hayupo nchini, Kotei ameendelea kuifuatilia klabu ya Simba na akidhirisha kuwa mabingwa hao wa nchi wako kwenye damu yake

Mwezi Januari alikataa kujiunga na Yanga akitoa sababu kuwa kufanya hivyo ni kuwasaliti mashabiki wa klabu ya Simba ambao wanamuheshimu sana

Post a Comment

0 Comments