BETI NASI UTAJIRIKE

KIUNGO WA MTIBWA SUGAR ATAKA KUTUA YANGA MSIMU UJAO



Kiungo wa Mtibwa Sugar, Abdulhalim Humoud, ameweka bayana kuwa anajisikia furaha kusikia kuwa anahusishwa na kujiunga na Yanga kutokana na ukubwa wa timu hiyo hapa nchini.

Humoud katika mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar na kumalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0, baada ya mchezo huo alionekana akiwa amevaa jezi ya Yanga na kwenda kupiga picha na mashabiki wa timu hiyo ambao walimshangilia.

Humoud amesema kuhusishwa kujiunga na Yanga kwake anajisikia faraja kubwa kwa kuwa Yanga ni timu kubwa hana tatizo la kucheza Jangwani.

Kuhusu tetesi za mimi kutakiwa na Yanga najisikia faraja sana kwa kuwa Yanga ni timu kubwa sana hapa nchini, na kama ambavyo unafahamu hakuna mfanyakazi ambaye hapendi kufanya kazi sehemu kubwa na mimi ni mfanyakazi, hivyo napenda kufanya kazi sehemu kubwa.

“Kwa sasa nipo Mtibwa Sugar, naishi vizuri na nayafurahia maisha ya hapa, hivyo ni ngumu kusema kuwa nataka labda kuondoka Mtibwa baada ya msimu huu kumalizika, tusubiri muda utaongea,” amesema kiungo huyo.

Post a Comment

0 Comments