BETI NASI UTAJIRIKE

MIQUISSONE AFUNGUKA MIPANGO YAKE NDANI YA SIMBA



Kiungo mshambuliaji wa Simba Luis Miquissone amesema mabao matatu aliyofunga mpaka sasa ni mwanzo tu wa safari ya mafanikio ambayo anataka kuitengeneza pale Msimbazi
Miquissone amesajiliwa na Simba dirisha dogo akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo hata hivyo ilikuwa imemtoa kwa mkopo UD Songo ya Msumbiji

Licha ya kuanza taratibu maisha yake ya soka nchini, kwa sasa Miquissone ni mchezaji tegemeo kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa nchi.Mwenyewe amesema hakuwa na mwanzo mzuri kwa kuwa alijiunga na Simba wakati akiwa likizo baada ya Ligi Kuu ya Msumbiji kumalizika

"Nilikuja hapa nikitoka likizo kule Msumbiji ligi ilikuwa imemalizika. Nashukuru baada ya kufanya mazoezi na timu nimeanza kuimarika ingawa bado sijafika pale nitapotaka, " amesema
"Malengo yangu ni kuisaidia Simba kwa kuifungia mabao mengi. Nimefunga mabao matatu lakini naona nina nafasi ya kufunga mabao mengi mechi zilizobaki kumaliza msimu"
Miquissone amejipambanua kwa kuwa mchezaji wa aina yake
Ana kasi, nguvu na silaha yake kubwa zaidi ni uwezo wake wa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha

Post a Comment

0 Comments