EYMAEL HAIOGOPI KABISA DERBY YA SIMBA NA YANGA ,Kesho Jumapili March 08, kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael anakabiliwa na mtihani wake wa kwanza wa mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Taifa

Eymael alijiunga na Yanga mwezi Januari 2020 siku chache baada ya kupigwa mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.Wakati Yanga ikicheza mechi ya kwanza ilikuwa ikisimamiwa na kocha Charles Mkwasa ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa mabingwa hao wa kihistoria

Inafahamika michezo ya dabi huongoza kuwaweka makocha na wachezaji matatani lakini Eymael amesema anakwenda kuikabili Simba bila presha yoyote.Mbelgiji huyo aliyefanya kazi mataifa mbalimbali barani Afrika, ametamba kuwa na uzoefu wa michezo ya aina hiyo

Pamoja na kufanya kazi kwa muda mrefu ligi kuu ya Afrika Kusini, Eymael amewahi kuionoa klabu ya AS Vita inayoshiriki ligi kuu ya DR Congo Wakati yuko Congo mchezo wake mkubwa wa dabi ulikuwa dhidi ya TP Mazembe

Lakini pia amewahi kuinoa AFC Leopards ya Kenya ambayo ina upinzani mkali na klabu ya Gor Mahia mchezo baina ya timu hizo ukipachikwa jina la 'mashemeji dabi'. Huu ndio mchezo mkubwa zaidi kwa ligi ku ya Kenya

Akiwa Sudan aliinoa klabu ya Al Hilal ambayo ina upinzani mkubwa na klabu ya El Marrikh, mchezo baina ya timu hizo ukiwa ndio mchezo mkubwa zaidi nchini Sudan.

Eymael amesema kuelekea mchezo huo haangalii matokeo ambayo wapinzani wake wamepata michezo ya nyuma, anaiandaa timu yake kimbinu ili kuweza kuibuka na ushindi

Post a Comment

0 Comments