advertise with us

ADVERTISE HERE

MAHADH AZUNGUMZIA KUREJEA DIMBANI NA MIPANGO YAKE NDANI YA YANGAKiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi bado anaendelea kufanya mazoezi binafsi kabla ya kuanza program za mazoezi na wachezaji wengine
Mahadhi aliumia mwezi August mwaka 2018 kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho hatua ya Makundi dhidi ya USM Alger, mchezo ambao Yanga iliondoka na ushindi wa mabao 2-1
Winga huyo mwenye kasi ya kimbunga, amesema haamini kama jeraha hilo limemuweka nje kwa miaka miwili.Hata hivyo anashukuru hali yake imetengemaa na karibuni ataanza kuonekana kikosini

"Nashukuru nakaribia kurejea dimbani kwa uwezo wa Mwenye ez Mungu. Nawashukuru sana wale walionipa msaada wa mawazo, fedha na hata chakula Mungu awabirik sana sina cha kuwalipa zaidi ni kunisubiria uwanjani inshaallah"

Hivi karibuni Mahadhi alianza mazoezi mepesi ya uwanjani ikiwa ni dalili njema kwake kuwa anakaribia kuwa fiti kuendelea na majukumu yake

Post a Comment

0 Comments