HIVI NDIVYO KOTEI ANAVYOWATEKA MABOSI WA SIMBAKwa siku za karibuni kiungo wa zamani wa Simba James Kotei amekuwa akitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutupia picha mbalimbali zikimuonyesha wakati yuko Simba
Ni msimu mmoja umepita tangu mwamba huyo kutoka Ghana alipoondoka Msimbazi kuelekea Afrika Kusini ambako alijiunga na klabu ya Kaizer Chiefs

Hata hivyo baada ya kukosa nafasi Chiefs Kotei alivunja mkataba wake wa miaka mitatu baada ya miezi sita tu na kuelekea barani Ulaya nchini Belarus ambako alijiunga na klabu ya Slavia Mozyr ambayo nayo bado hajapata nafasi kwenye kikosi cha timu hiyo
Kumekuwa na maoni tofauti miongoni mwa mashabiki wa Simba ambapo wapo wanaotamani kumuona Kotei akirejeshwa Msimbazi

Wakati kukiwa na tetesi kuwa Simba inamuwania kiungo mkabaji nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi, wapo wanaodhani kuwa nafasi hiyo ingemfaa zaidi Kotei kwani ni mchezaji anayeimudu vyema

Kotei pamoja na kumudu kucheza kiungo mkabaji, anao uwezo wa kucheza nafasi ya ulinzi wa kati na ndio maana wakati yuko Simba Jonas Mkude alicheza kwa uhuru zaidi kwani kazi zote za ulinzi zilikuwa zikifanywa na kotei

Kotei ni mchezaji mwenye mapenzi makubwa kwa Simba. Alidhihirisha hilo kwa kukataa kujiunga na Yanga mwezi Januari kwenye usajili wa dirisha dogo
Je mdau unadhani ni wakati muafaka kwa Simba kumrejesha Kotei?

Post a Comment

0 Comments