HILI HAPA GARI JIPYA LA CRISTIANO RONALDO BEI YAKE NI BILIONI 20Mshambuliaji wa Juventus na timu ya Taifa Ureno Cristiano Ronaldo anazidi kuweka rekodi duniani kwa kuwa mchezaji anayemiliki gari la bei kubwa zaidi ulimwenguni. 

Hivi karibuni kampuni ya Bugatti itaazimisha miaka 110 tangu kuanzishwa kwake na imetangaza ujio wa gari jipya liitwalo Bugatti Centodieci lenye thamani ya dola za kimarekani milioni 9 sawa na Bilioni 20 za kitanzania.

MUONEKANO WA MBELE WA BUGGATI CENTODIECI


MUONEKANO WA NYUMA WA BUGGATI CENTODIECI BEI YAKE NI BILIONI 20 ZA KITANZANIA

Cristiano Ronaldo ni mmoja ya watu 10 waliotoa oda ya gari hilo na Bugatti wamesema watatengeneza magari 10 tu.Hapo awali ilisemekana Ronaldo amenunua gari ghali zaidi liitwalo Buggati La Voiture Noire lenye thamani ya dola za kimarekani milioni 18 sawa na bilioni 40 za kitanzania lakini msemaji wa mchezaji huyo alikanusha taarifa hizo.

Ronaldo atapokea gari lake hilo mwaka 2021. Mbali kumiliki Bugatti Centodieci Ronaldo anamiliki Bugatti Chiron lenye thamani ya bilioni 7 ,Bugatti grand sport lenye thamani ya bilioni 5

BUGGATI VEYRON GRAND SPORT LINALOMILIKIWA NA RONALDO BEI YAKE NI BILIONI 5 ZA KITANZANIA 


RONALDO AKIWA GARI LAKE AINA YA BUGATTI CHIRON  LENYE THAMANI YA BILIONI 7 ZA KITANZANIA 

Post a Comment

0 Comments