Kocha mkuu wa timu ya taifa Tanzania Etienne Ndayiragijje ametangaza rasmi kikosi cha wachezaji 35 watakaotumika kwenye michuano ya kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Tunisia na kushiriki CHAN 2020 nchini Cameroon mwezi April Kikosi hicho cha wachezaji 35 kitaingia kambini tarehe 12-03-2020 kujiandaa na michuano hiyo huku baadhi ya nyota wakitemwa na kocha huyo akiwemo Juma Kaseja. Bodi ya ligi imetangaza kusimama kwa ligi kuu Tanzania bara kuanzia tarehe 12 na itarejea tena mara baada ya michuano ya CHAN kumalizika. Hii ni Orodha ya wachezaji 35 watakaotumika kwa michuano hiyo huku wengine wataondolewa kabla ya safari ya kuelekea Cameroon.
0 Comments