BETI NASI UTAJIRIKE

HATIMAYE GSM WAMWAGA MAMILIONI YA AHADI



Habari njema ni kuwa wachezaji wa Yanga tayari wamepata mgao wao wa Tsh Milioni 200 walizoahidiwa baada ya kuifunga Simba.Kulikuwa na maswali mengi kuhusu kuchelewa kwa mgao huo ambapo Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli alilazimika kutoa ufafanuzi wa mchakato wa fedha hizo

Bumbuli alisema utaratibu wa utolewaji wa fedha hizo ni tofauti na utaratibu waliokuwa wakiutumia kutoa Tsh Milioni 10 papo kwa hapo
"Milioni 200 ni fedha nyingi haziwezi kuwa na utaratibu sawa na Tsh Milioni 10. Kuna mambo tunapaswa kuyaweka sawa kabla ya kuwapa wachezaji mgao wao," alisema\

Ahadi ya Tsh Milioni 200 ilitolewa na wadhamini wa Yanga kampuni ya GSM, ikiwa ni hamasa kwa wachezaji ili waweze kushinda mchezo dhidi ya Simba
Wachezaji walipambana kupata ushindi wa bao 1-0, ushindi huo uliwapa furaha mashabiki wao ambao hawakuwa wameshangilia ushindi dhidi ya Simba tangu mwaka 2016

Post a Comment

0 Comments