Imeelezwa kuwa mkataba wa kiungo wa timu ya Yanga, Feisal Salum bado ni mrefu jambo linalowapa wakati mgumu timu zinazoiwinda saini yake kuipata saini yake kwa sasa.
Inaelezwa kuwa mabosi wa Simba walikuwa wakimpigia hesabu nyota huyo ambaye ameanza kurejea taratibu kwenye ubora wake.
Kwenye mchezo wa watani wa jadi uliochezwa Machi 8. Uwanja wa Taifa wakati Simba ikikubali kichapo cha bao 1-0 Fei aliwapa tabu viungo wa Simba wakiongozwa na Clatous Chama.
Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM lakini pia akiwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, amesema mkataba wa Feisal bado haujamalizika na hata kama ungekuwa unamalizika wasingekubali kumuachia.
Aidha, Hersi amewahakikishia wanachama na mashabiki wa Yanga kuwa wamejipanga kujenga kikosi imara, hivyo hawatakuwa na masihara kwenye usajili wa nyota watakaoitumikia Yanga msimu ujao.
“Wanayanga waondoe hofu, Feisal anabaki Yanga haendi popote pale mkataba wake ukimalizika tutamuongezea mwingine,” alisema Hersi.
Imeelezwa Feisal alisaini mkataba wa miaka mitatu wakati akijiunga na Yanga mwaka 2018, hivyo mkataba wake utamalizika mwaka 2021.
0 Comments