kiungo mshambuliaji wa Simba Francis Kahata amesema kuwa wana kazi kubwa na ngumu ndani ya Ligi Kuu Bara kusaka pointi tatu kwa kuwa ndiyo malengo waliyojiwekea. Kahata amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Simba baada ya kujiunga msimu huu wa 2019/20 akitokea klabu ya Gormahia ya Kenya amehusika kwenye jumla ya mabao 10 ya Simba kati ya 55 akifunga mabao manne na kutoa pasi za mwisho sita. Kahata amesema: "Kuna kazi kubwa ya kufanya ndani ya ligi, mechi zimekuwa ngumu na ushindani ni mkubwa lakini hatuna namna ni lazima tupambane kupata pointi tatu na hayo yote yanawezekana kwa kuwa tunashirkiana. "Kushindwa kufikia malengo inaumiza na hilo lipo wazi, tunaomba sapoti ya mashabiki kwani wao wanatupa nguvu," Machi 8, Simba itakaribishwa na Yanga Uwanja wa Taifa kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa pili, kwenye mchezo wa kwanza waliocheza Januari 4, timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments