BETI NASI UTAJIRIKE

EYMAEL AUZUNGUMZIA USHINDI WA 8-0 KWA SIMBA


Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael ambaye ndiye mwenye kauli ya mwisho kwenye benchi la ufundi la Yanga, amefunguka kuwa wapinzani wao Simba ni timu bora.
Kocha huyo raia wa Ubelgiji, ameweka bayana kwamba Simba ni timu bora kwa sababu licha ya kwamba waliwafunga kwa bao 1-0 lakini mechi yao iliyofuata waliibuka tena na wakashinda kwa mabao 8-0 tofauti na wao ambao walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya KMC.
Eymael amesema kuwa ubora wa Simba ulionekana baada ya kuwafunga lakini wakasimama na kufanya vizuri kwenye mechi yao iliyokuja katika ligi kuu.  
“Licha ya kwamba sisi ndiyo tuliwafunga Simba, lakini wao walivyofanya baada ya kupoteza mechi yetu ni kusimama na kusonga mbele kushinda kisha wakaja kupata ushindi wa mabao 8-0.
“Hii ni ishara ya timu bora na sisi tunatakiwa tufanye hivyo kwenye mechi zetu zijazo ingawa mechi ya kwanza baada ya kuwafunga na KMC tuliipoteza,” alisema Mbelgiji huyo.

Post a Comment

0 Comments