BETI NASI UTAJIRIKE

EYMAEL AMPA MBINU MORISSON NAMNA YA KUIMALIZA SIMBA


kiungo mshambuliaji wa Yanga Benard Morrison amepewa kazi maalumu ya kuiua Simba watakapokutana Machi 8 Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.Mchezo wa kwanza uliowakutanisha Simba na Yanga Januari 4, timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 mchezo huo Morrison aliukosa.Akizungumza na www.amospoti.com, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa anamtazama Morrison kiupekee licha ya tabia yake ya kupenda kuchezea mpira kukaa kichwani mwake ila anaamini atafanya makubwa kwenye mechi yao dhidi ya Simba.
Kitu kimoja alichonacho Morrison na kinanishangaza ni uwezo wa kufanya maamuzi kwa haraka na kuwa na jicho la mpira, kwa mwenendo anaokwenda nao itakuwa rahisi kutupatia matokeo mbele ya Simba kazi yake itakuwa moja tu kutazama mipira kwa jicho la kipekee kabla ya kugawa kwa wengine.
“Mechi zetu alizocheza amekuwa akitengeneza nafasi nyingi lakini wenzake wanashindwa kuzitumia jambo ambalo linamkasirisha hata yeye ila nitakaa naye na kuzungumza naye kwa kina kutatua tatizo hili,” amesema

Post a Comment

0 Comments