advertise with us

ADVERTISE HERE

EPL YAPIGWA KALENDA TENA , TATHMINI ZAONYESHA HASARA NI ZAIDI YA TRILIONI 2Mara baada ya tarehe ya kurejea kwa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ kusogezwa mbele kutoka Aprili 4 hadi Aprili 30, kutokana na hofu ya Ugonjwa wa COVID-19 unaotokana na Virusi vya Corona, imebainika kuwa kuna gharama kubwa nyuma yake.

Ligi hiyo ambayo ina mikataba mingi inaweza kuwapa hasara uongozi wa Premier League kama itatokea ligi hiyo itashindwa kurejea kama kawaida. 

Imeelezwa kuwa gharama ya kutomalizika kwa ligi hiyo kutasababisha uongozi wa Premier ulipe pauni 762m (zaidi ya Sh trilioni 2) kama malipo ya kuvunjwa kwa mkataba wa kutomalizika kwa msimu wa 2019-20.
Ligi hiyo na nyingine zote zimesimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimekuwa vikisambaa kwa kasi nchini England huku kukiwa hakuna tiba iliyopatikana.

Vituo ambavyo vimelipia malipo ya msimu mzima ikiwemo Sky Sports vinahaha kuhakikisha mikataba ya matangazo inawekwa sawa kwa kuwa malipo yameshafanyika na mambo hayajaenda sawa. Malipo ya haki za matangazo huwa yanafanyika mapema na baadhi huwa yanatolewa kwa klabu mwanzoni mwa msimu.

Njia pekee ambayo inaweza kupunguza makali ya kulipa fidia hiyo ni michezo kuendelea kwa kuchezwa bila mashabiki ili angalau yale makampuni yaliyolipia haki za matangazo yasiishitaki Premier League. Klabu zinahitaji malipo ya haki za kuonyeshwa kwa michezo yao ili ziwasaidie katika malipo ya mishahara ya wachezaji wao wakati huu ambapo ligi zimesimama

Post a Comment

0 Comments