DYBALA,FELLAINI NA MALDINI WAKUTWA NA JANGA LA CORONAMshambuliaji wa klabu ya Juventus nchini Italia Paul Dybala amekumbwa na janga la Corona. Dybala anakuwa ni mchezaji wa tatu kutoka Juventus kukutwa na maambukizi hayo . Dybala na Mchumba wake walikutwa na maambukizi hayo na walijitokeza hadharani kujitangaza. 

Kupitia Instagram Dybala aliandika "Habari, Nataka kuwajulisha mimi na Oriana tumekutwa na maambukizi ya Covid-19 kwa bahati nzuri tunaendelea vizuri.santeni kwa meseji zenu"

Nchi ya Italia inaongoza kwa wingi wa waathirika na vifo  baada ya kufikisha vifo 5,476 huku ikiweka rekodi ya vifo 651 kwa siku moja. 

Beki wa Zamani wa Italy na AC Milani Paul Maldni na yeye ni mmoja wa wahanga wa Coron baada ya vipimo kuonyesha amekutwa na virusi.Maldini anaungana na nyota wa zamani aliyekipiga Manchester united Marroune Fellaini aliyekutwa na virusi hivyo hapo jana akiwa nchini China.


Post a Comment

0 Comments