BETI NASI UTAJIRIKE

VIONGOZI,MAKOCHA ,WACHAMBUZI WAZUNGUMZIA KIWANGO CHA LUIS MIQUISONNE SIMBA



Dakika  600 alizocheza Luis Jose ndani ya Simba, zimempoteza kabisa Shiza Kichuya waliyesaini nae kwenye dirisha dogo. Lakini kiwango chake kimewapa kiburi viongozi wa Simba ambao wamesisitiza kwamba wanataka mashine zingine kama yeye na tayari wameshaanza kazi hiyo kusuka kikosi cha mashindano ya kimataifa

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema anajivunia usajili wa Luis kwenye dirisha dogo na tayari wameanza kusaka mastaa wapya ambao lazima wawe na kiwango chake au kumzidi na wenye umri mdogo kama wake pia

Kichuya ambaye alikuwa na jina kubwa ndani ya Simba kutokana na bahati yake ya kuifunga Yanga kabla hajaenda Misri,ameshindwa kushawishi benchi la ufundi kumpa jezi hata ya kukaa kwenye benchi.

Kichuya alibahatika kucheza mechi mbili tu moja ya Ligi na nyingine ya FA ambazo nazo hakumaliza dakika 90 dhidi ya Stand United dakika 54 na JKT Tanzania dakika 45
Luis ambaye awali alikuwa hayumo sana midomoni mwa mashabiki wa Simba, michezo aliyocheza ambayo alipewa dakika zote 90 ni pamoja na mechi dhidi ya JKT

Tanzania,baada ya hapo alikosa michezo mitatu mfululizo, baadae akapewa dakika moja tu dhidi ya Mtibwa. Pia alikosa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Stand United ugenini,baada ya hapo Luis hajakosa tena mchezo wowote kati ya sita iliyochezwa hadi sasa akiwa ameingia kambani mara tatu

Michezo hiyo ni dhidi ya Kagera Sugar ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0 yeye akiingia kambani alicheza dakika 79. Alihusika kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Biashara akifunga bao moja baada ya kucheza dakika zote 90 namchezo dhidi ya KMC alifunga bao zote mbili kwenye ushindi wa 2-0 akicheza dakika 76, alicheza tena na Azam na timu yake iliibuka na ushindi wa bao 3-2 alicheza dakika 84

Luis alicheza tena dhidi ya Yanga ambapo walikubali kichapo cha bao 1-0 alicheza dakika zote 90 na mchezo wake wa mwisho ni dhidi ya Singida United ambapo timu yao ilipata ushindi mkubwa wa mabao 8-0 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam alicheza dakika zote 90

Mchambuzi wa soka nchini, Licky Abdallah ‘Dk Licky’ amesema;
"Kwenye timu hakukosekani staa wa timu kulingana na ubora ikiwa ni sambamba na namna anavyopambana kuisaidia timu yake kupata matokeo kwa nyota huyo sasa amefanikiwa kufanya hivyo kutokana na kila mtaa kuzungumzwa ni kutokana na ubora wao."

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay amesema, Luis anapokuwa na mpira anakuwa mzuri zaidi na mchango wake unaonekana na uwanjani anacheza akiwa huru, lakini timu inapokuwa haina mpira uwezo wake wa kukaba ni mdogo.
Alisema, ubunifu wake awapo uwanjani, ndio umekuwa ukiwasababishia mabeki wa timu pinzani kuwachezea madhambi zaidi anapokuwa na mpira.

Naye Kocha wa JKT Tanzania, Abdallah Mohammed ‘Bares’ alisema ni fundi anacheza mpira wa kisasa unaotakiwa duniani. Ni msaada kwenye timu, juhudi zake binafsi zinambeba na hii ni kwa sababu anajua kuchezea mpira

Post a Comment

0 Comments