BUNDI WA VIPIGO ATUA LIVERPOOL KILA MTU ANAJIPIGIA APENDAVYO


Klabu ya Liverpool imeendelea kupokea kipigo cha tatu kwa mwaka 2020 kutoka kwa Chelsea kwenye michuano ya FA. Awali Liverpool ilikuwa inashikilia rekodi ya kutofungwa kwenye michuano mbalimbali ikiwamo ligi kuuu Uingereza lakini kwa ssa wanafungika kirahisi mno

Liverpool wanaondoshwa kwenye michuano ya FA kwa msimu huu na Chelsea hivyo kuwafanya kugombea makombe mawili tu mpaka sasa likiwemo lile la Champions League ambapo wanakibarua kizito cha kuwafunga na kuwaondoa Atletico lakini pia wanapaswa kushinda michezo iliyobaki ligi kuu Uingereza

Zifuatazo ni sababu za Liverpool kufungwa mechi 3 mfululizo

1.Ubovu wa safu ya ushambuliji hasa wanapokutana na timu yenye safu imara ya ulinzi. Hili limejitokeza kwenye mechi mbili kati ya Liverpool vs Atletico madrid ambapo Liverpool walimiliki mpira lakini hawakufanikiwa kuiga shuti lililolenga golini huku udhaifu huo ukionekana kwenye mchezo dhidi ya Watford baada ya kupiga shuti moja tu kwenye lango la atford na kuambulia kipigo cha mabao 3-0

2. Ugomvi wa Salah na Mane. Ugomvi huu tangu kuzuka kati ya wachezaji hawa wawili umesababisha klabu hiyo kutopata ushindi wa uhakka . Mane na Salah ni wachzji walikuwa wanaunda safu y hatari lakini ugomvi wao wa nje ya uwanja umehaibu urafiki wao na ushirikiano ndani ya uwanja 


Post a Comment

0 Comments