Bodi ya ligi kuu imetangaza kuunga mkono uamuzi wa Serikali kusitisha shughuli zote za michezo kwa mwezi mmoja ili kudhibiti maambukizi ya visusi vya Corona
Katika kikao kilichofanyika leo, Bodi imeazimia mambo kadhaa ili kuhakikisha baada ya muda uliowekwa na Serikali kupita, Ligi inaendelea katika mazingira salama
Bodi imeweka maazimio manne ikiwamo ligi kuchezwa bila mashabiki baada ya siku 30 za kusimamishwa kwa mashindano yote nchini.
Ofisa Mtendaji wa Bodi (CEO), Almas Kasongo amesema katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Corona ulioingia nchini, wameazimia Ligi kuchezwa bila mashabiki itakapoendelea mwezi ujao.
"Tumeweka maazimio manne, Serikali ikijiridhisha hali ni shwari nchini na kuruhusu Ligi kuendelea, basi wachezaji wote watapimwa kabla ya mechi," alisema.
Aidha, Bodi imeazimia kuwa ligi imalizike ndani ya mwezi Juni ili kutoa nafasi kwa timu zitakazoiwakilisha nchi kimataifa kuendelea na mchakato wa mashindano ya CAF.Lakini pia Bodi itaendelea kusimamia afya kipindi hiki cha tahadhari ya Corona
0 Comments