Mhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema kikosi cha timu hiyo kiko tayari kwa mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa.Msemaji huyo wa Yanga amesema kocha Luc Eymael tayari ameandaa mbinu za kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo
Nugaz amesisitiza kuwa Yanga haitaingia kama 'undar-dog', wanatambua kuwa Simba ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri lakini siku hiyo watakumbana na Yanga ambayo hawajawahi kuiona
"Sisi hatutaingia kama under-dog kama wanavyosema wengine, tunaiheshimu timu yao pamoja na wachezaji wao lakini siku hiyo tutawachezea mpira ambao hawajawahi kuuona," ametamba Nugaz
"Tunafahamu udhaifu wao uko wapi ndio maana hata kocha wetu amesema hana wasiwasi kabisa kuwakabili Jumapili.Mashabiki wetu waje uwanjani kwa wingi, wajiamini na watembee kifua mbele kwani siku hiyo Mnyama hana pa kutokea"
Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa kocha Luc Eymael na anaweza kuweka rekodi mpya kama ataiongoza Yanga kupata ushindi
Baada ya password ya ushindi kuletwa na Jerry Muro, pengine siku ya Jumapili itakuwa siku ya furaha kwa mashabiki wa Yanga
0 Comments