Ukizungumzia wachezaji wenye muda mrefu kwenye kikosi cha Yanga, kiungo mshambuliaji Deus Kaseke ni miongoni mwao
Kaseke alijiunga na Yanga msimu wa 2014/15 akitokea klabu ya Mbeya CIty, baadae akaondoka kwenda kuitumikia Singida United kwa msimu mmoja kabla ya kurejea Jangwani
Alikuwa kwenye kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa wa ligi kuu kwa misimu mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2014
Ndio! kwa wale wanaodhani kutwaa taji la ligi kuu mara tatu mfululizo ni jambo jipya, wachukue kumbukumbu hii
Baada ya Saimon Msuva kuondoka, Kaseke alionekana kama miongoni mwa wachezaji ambao wangeweza kuzipa nafasi yake, lakini haikuwa hivyo kiwango cha Kaseke kimekuwa kikipanda na kushuka, wakati mwingine hatabiriki
Baada ya Zahera kuondolewa na Mkwasa kukabidhiwa timu, Kaseke alikuwa 'wa-moto' kwelikweli alitengeneza nafasi kwenye kila mchezo alioshuka dimbani
Hata hivyo tangu ujio wa Luc Eymael, mambo yamekuwa tofauti kwa upande wake, yale makeke yake yamepungua pamoja na kuwa anapata nafasi ya kucheza
Kaseke ni mmoja wa wachezaji mahiri kwenye kikosi cha Yanga, lakini nadhani kuna kitu anapaswa kufanya ili arejeshe makali yake
Kwani kama Kaseke yule wa wakati ule angekutana na huyu Morrison, Yanga isingekuwa inapata tabu kufunga mabao
0 Comments