Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ameondoka nchini juzi kuelekea Ubelgiji kushughulikia masuala binafsi.Eymael anatarajiwa kufunga ndoa March 28 huko Ubelgiji
TFF ilitahadharisha kuwa wageni wanaosafiri wakati huu wa janga la Corona wanaweza wasiruhusiwe kurejea nchini kama Serikali itachukua hatua ya kufunga mipaka
Hata hivyo, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema watachukua hatua za kiusalama kwa wageni wote waliosafiri pale watakaporejea
Amesema watafanyiwa vipimo vya Corona kuhakikisha wako salama kabla ya kuwaruhusu kuchanganyika na wengine kuendelea na majukumu yao
0 Comments