Wakati huu Ligi ikiwa imesimama baada ya Serikali kuchukua tahadhari kudhibiti maambukizo ya ugonjwa wa Corona, Simba pamoja na timu zote zinazoshiriki ligi kuu zimewapa wachezaji mapumziko kuwatenga ikiwa ni agizo lililotolewa na Serikali kuzuia mikusanyiko ya aina yoyote kwa muda wa siku 30
Sasa kwa upande wa Simba wachezaji walipewa program maamum za mazoezi ambayo wanapaswa kuyafanya huko makwao.Hili ni suala la mchezaji kujisimamia yeye mwenyewe lakini uongozi wa Simba umebanisisha kuwa watawabaini wachezaji ambao watapuuzia program hizo
Moja ya mikakati iliyowekwa ni kuwa watakaporeja, kila mchezaji atapimwa utimamu wake wa mwili hivyo kwa wale ambao hawatakuwa 'fit' watawajibishwa
Ligi bado haijakamilika raundi 10 za mwisho Simba ikiwa inaongoza msimamo baada ya kujikusanyia alama 71
Simba itahitaji kushinda mechi tano tu ili kutetea ubingwa wake kwa msimu wa tatu mfululizo
0 Comments