BETI NASI UTAJIRIKE

NUGAZ: TULETEENI HAO SIMBA TUWAFUNGE TENA FA




Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema hawana hofu kabisa na watani zao Simba na wako tayari kukutana nao tena kwenye michuano ya kombe la FA ambayo droo ya hatua ya robo fainali iliahirishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona

Nugaz amesema wanaweza wasiwe na mwenendo mzuri sasa lakini haimaanishi kuwa wakikutana na Simba watafungwa

"Hawa tukutane nao hata mara 10 msimu huu, bila ya makandokando hawatufungi ng'o!," alitamba Nugaz'

"Tena itakuwa vyema tukutane nao kwenye kombe la FA tuwaonyeshe kwa nini sisi tunabaki kuwa mabingwa wa kihistoria Tanzania"

Pamoja na mabadiliko makubwa ya kikosi chake, msimu huu Yanga imezima tambo za watani zao Simba baada ya kuondoka na alama nne kati ya sita dhidi yao kwenye ligi
Ni kutokana na matokeo ya sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa pili uliopigwa March 08

Upo uwezekano miamba hiyo ya soka nchini ikakutana kombe la shirikisho la Azam kama wote wataweza kutinga fainali au droo ikawakutanisha mapema

Post a Comment

0 Comments