BETI NASI UTAJIRIKE

SENZO AZUNGUMZIA MKATABA MPYA KWA KONDE BOY "MIQUISSONE"


Ukiondoa nyota ambao mikataba yao imemalizika na wana sifa za kuongezewa mikataba mipya, wachezaji wapya watakaosajiliwa watasaini mkataba wa kuanzia miaka mitatu au zaidi

Ni utaratibu ambao klabu ya Simba imejiwekea ili kuwa na uhakika wa huduma za wachezaji wake kwa muda mrefu
Luis Miquissone aliyetua dirisha dogo, ni mchezaji wa kwanza kuanza na utaratibu huo baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa pia amesema watazingatia umri kwa nyota ambao wanawasajili

"Tunataka kuwa na kikosi ambacho kitakuwa na sisi kwa muda mrefu kama ambavyo tumefanya kwa Luis Jose, tutakuwa tunasajili wachezaji vijana lakini pia sio kila kijana bali kijana ambaye ana vigezo vya kucheza Simba," alisema Senzo

"Ukiwa na mchezaji kijana ambaye amesaini miaka mitatu na akiwa bora unakuwa na uhakika wa kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa"

Simba inaendelea na mchakato wa kuwaongezea mikataba nyota wake huku wakiendelea na mchakato wa kusaka nyota wapya ambao watasajiliwa mwezi Juni

Post a Comment

0 Comments