BETI NASI UTAJIRIKE

MIRAJI ATHUMAN AZUNGUMZIA MAENDELEO YA AFYA YAKE



Baada ya kukaa nje kwa zaidi ya miezi mitatu kutokana na majeraha, hatimaye mshambuliaji wa Simba Miraji Athumani anatarajiwa kuanza mazoezi wiki ijayo
Msimu huu Miraji amecheza mechi 10 tu, lakini amefunga mabao sita na kutoa asisti mbili
Nyota huyo aliyerejea akitokea klabu ya Lipuli Fc, amewashukuru mashabiki ambao wameendelea kuulizia maendeleo yake

"Mimi naendelea vizuri nilipata majeraha chini ya mguu wa kulia mfupa ulipata ufa, yamenitesa sana lakini sasa nashkuru madaktari wamenisaidia, wameniambia naweza kuanza mazoezi mepesi baada ya siku nane," alisema Miraji
"Mazoezi nitakayoanza nayo ni kunyonga baiskeli, baadae ndio nitaanza ya uwanjani taratibu"

Upo uwezekano mkubwa Miraji ataanza kuonekana dimbani baada wiki mbili mpaka tatu

Post a Comment

0 Comments