BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA KURUDI KAMBINI JUMANNE YA TAREHE 31



Wakati wachezaji wa timu ya Wanawake na ile ya vijana wakiendelea kubaki nyumbani, uongozi wa Simba umewaagiza wachezaji wake wa kikosi cha kwanza kurejea kabla ya March 31, imefahamika

Kufuatia Serikali kusitisha shughuli zote zenye mikusanyiko kwa muda wa siku 30, Simba kama zilivyo timu nyingine zilitoa mapumziko kwa nyota wake ambapo awali wachezaji wa kikosi cha kwanza walipewa wiki moja ya mapumziko wakati timu ya Wanawake na ile ya vijana wakipewa wiki mbili

Hata hivyo ni kama muda huo uliongezwa lakini sasa Simba imewaagiza wachezaji wa kikosi cha kwanza warejee


Tamko hili huenda likawaweka matatani wachezaji waliosafiri nje ya nchi kwani watakaporejea watahitaji kukaa karantini kwa muda wa siku 14 kulingana na agizo lililotolewa na Rais Dk John Magufuli

Lakini pia kwa nchi kama Rwanda huenda mshambuliaji Meddie Kagere akashinda kurejea mapema kwani nchi hiyo imezuia safari zote za ndani na nje huku wananchi wakizuiwa kutembea
Rwanda inatoa huduma za chakula, na mahitaji muhimu bure kwa watu wake

Post a Comment

0 Comments