DILUNGA AGEUKA DILI KIMATAIFAHassan Dilunga amekuwa na msimu mzuri ndani ya kikosi cha Simba na haishangazi kuona timu nyingi zimejitosa kumuwania.Mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu na inaelezwa vilabu kadhaa kutoka Misri na Afrika Kusini vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili

Dilunga ambaye ameifungia Simba mabao saba kwenye ligi, inaelezwa mkononi ana ofa kutoka klabu moja ya Afrika Kusini ambayo ilimtaka kwa ajili ya majaribio
Alishindwa kwenda wakati huu baada ya ligi hiyo kusimama kutokana na janga la Corona
Lakini Simba haiko tayari kumuona kiungo huyo akiondoka Msimbazi, inaelezwa mazungumzo ya mkataba mpya yanaendelea

Post a Comment

0 Comments