MAKAME AFUNGUKA KUKAA BENCHI NA MIPANGO YAKE NDANI YA YANGAKiungo Abdulaziz Makame 'Bui' alianza vyema maisha yake kunako klabu ya Yanga wakati wa kocha Mwinyi Zahera.Alikuwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha Yanga kilichoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa na baadae kombe la Shirikisho
Hata hivyo baada ya kuingia kocha Charles Mkwasa na baadae Luc Eymael, Makame ameshindwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza

Pengine ni kutokana na mabadiliko ya mfumo wa uchezaji ambapo makocha hao wamemrejesha nahodha Papy Tshishimbi nafasi ya kiungo mkabaji na hivyo kumfanya Makame akose hata nafasi ya kukalia benchi

Makame amesema pamoja na kuwa jambo hilo linamumiza, lakini amechukua kama changamoto ya kumfanya ajiimarishe zaidi

"Ni changamoto, lakini naamini kila jambo lina wakati wake, mdogo mdogo nitatimiza malengo yangu kwani sijioni kama nimefika na siku zote mwenye njaa ndiye anayetafuta sana," amesema

Hivi karibuni Makame aliingia matatani baada ya inayodaiwa kuwa ni sauti yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akilalamika kuwa hakupewa mgao baada ya ushindi dhidi ya Simba

Makame hakuwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 waliopata nafasi kwa ajili ya mchezo huo
Uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa kila mchezaji aliyesajiliwa amepata mgao wake ingawa kiasi walichopata kinatofautiana kulingana na ushiriki wa mchezaji

Post a Comment

0 Comments