BETI NASI UTAJIRIKE

EYMAEL NA MOLINGA WAKITUA TU KITUO CHA KWANZA NI KARATINI



Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela jana alikiri kuwa waliwaruhusu kusafiri kocha mkuu Luc Eymael na mshambuliaji David Molinga licha ya tishio la ugonjwa wa Corona

Molinga aliruhusiwa kwenda Ufaransa kushughulikia masuala binafsi wakati Eymael amekwenda Ubelgiji kufunga ndoa

Juzi TFF ilipiga 'mkwara' kuwa wachezaji na wafanyakazi wa kigeni waliosafiri kwenda nje ya nchi wakati huu, wanaweza wasiruhusiwe kurudi nchini na pengine kuzuiwa kushiriki ligi kuu pale watakaporejea

Lakini kwa tamko lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli hapo jana, wageni wataruhusiwa kuingia nchini lakini kuanzia jana wanapaswa kuwa chini ya uangalizi 'karantini' kwa siku 14

Serikali imethibitisha kuwa mpaka sasa watu 12 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona nchini hivyo wananchi wameaswa kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo

Post a Comment

0 Comments