BETI NASI UTAJIRIKE

MDAU: DKT MSOLA WATUMIE VIZURI WADHAMINI KUELEKEA MSIMU WA 2020/2021


Ni wazi msimu wa Yanga kwa upande wa ligi kuu umeshamalizika kwani hakuna tena nafasi ya kutwaa ubingwa kwa mechi zilizobaki.Umekuwa msimu uliokuwa na changamoto nyingi za ndani ya uwanja, kwani nje ya uwanja baada ya GSM kuingia, angalau mambo ya kifedha yamekaa sawa

Wakati mwingine tunapaswa kukubali hali halisi, mara chache mafanikio huja kwa bahati, lakini mara nyingi yanahitaji maandalizi

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla pamoja na timu yake ya uongozi, kwa kiasi kikubwa wamejitahidi kuiweka timu kwenye mazingira ya ushindani.Ujio wa GSM kama wadhamini ni juhudi zao, tumeona mabadiliko ya kikosi tangu wakati wa Zahera mpaka sasa Luc Eymael

Pengine mambo haya yalichelewa kufanyika kwani yamekuja wakati robo ya msimu ikiwa tayari imekatika

Bado kuna nafasi kwenye michuano ya kombe la FA (ASFC) huku ndiko ambako kipaumbele kinapaswa kuwekwa.Kwani ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao, Yanga inapaswa kutwaa taji la FA

Huku kuna mechi tatu muhimu, hizi ndizo mechi za kufa nazo.Yanga imedhihirisha ikiwa na jambo lake ikitaka liwe, linakuwa

Majuzi tu mkazo mkubwa uliwekwa kwenye mchezo dhidi ya Simba na ushindi ukapatikana
Nguvu hiyo sasa ihamishiwe kwenye FA, ingawa bado upinzani utakuwa mkubwa kwani huko nako wale watakaopangwa kucheza na Yanga pengine wataahidiwa mamilioni kama ulivyokuwa mchezo wa KMC!

Post a Comment

0 Comments