HAWA HAPA NYOTA WANNE YANGA WATAKAOIKOSA NAMUNGO FC LEO


Wakati Yanga leo ikitarajiwa kuumana na Namungo Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Majaliwa, baadhi ya nyota watakosekana kutokana na sababu mbalimbali

Mlinzi wa kushoto Adeyum Saleh alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya KMC, hakusafiri na timu kwa kuwa bado anauguza majeraha hayo ya goti
Mohammed Issa 'Banka' ni nyota mwingine ambaye ni majeruhi huku mkongwe Kelvin Yondani akiwa na matatizo ya kifamilia na Haruna Niyonzima ana kadi tatu za njano
Habari njema ni kuwa kiungo mshambuliaji Bernard Morrison anaweza kurejea baada ya hali yake kuimarika kwa haraka

Morrison alipata majeraha kabla ya mchezo dhidi ya Simba ambao alicheza kwa dakika 56 kabla ya kutolewa kumpisha Patrick Sibomana

Mchezo dhidi ya Namungo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na ukweli kuwa Namungo ni moja ya timu bora msimu huu.Ni mchezo ambao Yanga inahitaji matokeo ya ushindi hasa baada ya kupoteza mchezo uliopita

Post a Comment

0 Comments