BETI NASI UTAJIRIKE

TSHISHIMBI HAENDI KOKOTE, WADHAMINI WAMMWAGIA MAMILIONI



Moja ya wadhamini wa Yanga kampuni ya GSM jana ilifanya mambo mawili makubwa ya usajili
Kwanza walimaliza suala la Bernard Morrison baada ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili mbele ya ile miezi sita aliyokuwa amesaini mwezi Januari
Ni baada ya kubaini Simba ilianza kumshawishi nyota huyo kutoka Ghana asaini kwao
Lakini hawakuishia hapo, nahodha Papy Tshishimbi nae aliongezewa mwaka mmoja zaidi kwenye mkataba wake ambao ulikuwa umebaki mwaka
Mwezi Juni 2019 Tshishimbi alisaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Kama ilivyokuwa kwa Morrison, Tshishimbi alishaanza kuzengewa na vilabu vya Simba na Azam Fc
Jambo kubwa ambalo Yanga imedhamiria kulifanya msimu huu, ni kuhakikisha hawawapotezi nyota wao muhimu kwa timu nyingine
Msimu uliopita nyota watatu nahodha Ibrahim Ajib, Gadiel Michael na Beno Kakolanya walijiunga na Simba
Kwa miaka ya hivi karibuni klabu ya Simba imekuwa ikifanya jitihada za kuivuruga Yanga kwa namna yoyote iwe kwa kuwanunua wachezaji wao muhimu hata kama hawawahitaji au kuingilia kati usajili wowote ambao Yanga wanataka kuufanya
Awali Yanga ilikuwa ikishindwa kuwazuia wachezaji wake kutokana na changamoto za kiuchumi lakini kwa sasa uwepo wa GSM umerudisha jeuri ya Yanga kwenye usajili

Post a Comment

0 Comments