BETI NASI UTAJIRIKE

MDAU: KICHUYA HUU NI WAKATI SAHIHI WA WEWE KULIPA DENI LA SIMBA



Baada ya kurejea Simba akitokea klabu ya Pharco ya Misri, wengi tulikuwa na imani kubwa kwa winga Shiza Kichuya ambaye amewahi kuwafunga Yanga mara tatu mfululizo
Uzingumzia mafanikio ya Simba msimu wa 2016/17 na 2017/18 huwezi kukosa kutaja jina la Kichuya

Msimu wa 2017/18 Kichuya aliweka rekodi ya pasi za mabao. Kwenye msimu huo alitoa pasi 27 za mabao

Nadhani ni takwimu za juu sana kuwahi kuonekana kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara
Hata hivyo Kichuya wa sasa sio yule tunayemfahamu, ameshuka kiwango
Alisajiliwa pamoja na 'Mmakonde' Luis Miquissone, mwenzie moja kwa moja ameonyesha makali yake na kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza

Kichuya amecheza mechi mbili tu na kwa maoni ya kocha Sven Vandenbroeck, amemtaka aongeze juhudi ili aweze kumpa nafasi
Hakuna mwenye shaka na kipaji chake, pengine kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara huko Misri kumemfanya arudi nyuma
Bado anayo nafasi ya kuwadhihirishia Wanamsimbazi kuwa ubora wake bado upo palepale, na kuwa mechi zilizopita hakuwa kwenye 'form' tu

Post a Comment

0 Comments