Baada ya beki wa kati wa klabu ya Yaga Ally Ally kuvuta jiko wiki iliyopita jana ilikuwa ni zamu ya kocha wa timu hiyo raia wa ubelgiji Bw.Luc Eymael na Bi Patricia Abruzzese. Ndoa ya kocha huyo ilifungwa nchini Africa Kusini katika kanisa la Harre. Inaelezwa ndoa hiyo haikuhudhuliwa na watu wengi kutokana na katazo la serikali duniani kote kutokaa kwenye mikusanyiko ili kudhibiti kusambaa na kuenea kwa virusi vya COVID-19. Eymael amenukuliwa akisema "Ni kweli nimefunga ndoa lakini ilikuwa ni binafsi kwakua kuna mlipuko wa virusi vya Corona, tulienda kanisani tu tumemaliza tunashuru," Bi Patricia anakuwa ni mke wa tatu wa kocha huyo kwa mujibu wa maelezo yake aliyoyatoa hivi karibuni
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments