BETI NASI UTAJIRIKE

NUGAZ: YALE MAMILIONI YETU YANAANZA KUINGIA LEO KWENYE AKAUNTI


Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema siku ya leo wachezaji wote wa Yanga watawekewa fedha zao za mgao wa Tsh Milioni 200 walizopata baada ya kupata ushindi dhidi ya Simba Jumapili ya March 08 2020

Nugaz amesema mchakato wa mgao wa fedha hizo ulikamilika tangu juzi lakini zoezi la wachezaji kuwekewa fedha kwenye akaunti zao litafanyika kuanzia leo Jumatatu ambayo ni siku ya kazi

Jana Yanga ilicheza na Namungo Fc mchezo wa ligi kuu ambao ililazimishwa sare ya bao 1-1 huko Ruangwa wilayani Lindi
Kukosekana kwa nyota wengi kwenye kikosi cha Yanga wapo waliohusisha na 'mgomo' wa fedha hizo

Hata hivyo uongozi wa Yanga ulitoa ufafanuzi wa kukosekana kwa nyota wake sita ambapo ukiondoa Haruna Niyonzima (kadi tatu za njano), Lamine Moro, Mohammed Issa 'Banka' na Adeyum Saleh ambao ni majeruhi, Kelvin Yondani na David Molinga waliomba ruhusa kwa kuwa walikuwa na matatizo ya kifamilia

Kabla ya mchezo jana, Kocha Luc Eymael alitoa malalamiko kuwa baadhi ya nyota wake wamekuwa na tabia ya kujipangia mechi za kucheza
"Haiwezekani timu ina mchezo muhimu halafu mchezaji anagoma kusafiri, anasema ana matatizo ya kifamilia. Huku ni kuikosea heshima Yanga kwani wao wapo Yanga kwa kazi moja tu, kuipigania timu"

Post a Comment

0 Comments