NUGAZ: KAMA SIMBA WASIPOBEBWA TUTAWAFUNGA


Afisa Mhamasishaji na Msemaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema kikosi cha timu hiyo kimejipanga sawasawa kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa siku ya Jumapili, March 08 kwenye uwanja wa Taifa

Nugaz ametamba kuwa kwa maandalizi ambayo wamefanya, wana matumaini makubwa ya kupata matokeo katika mchezo huo na wakati huohuo akiwataka waamuzi wachezeshe kwa kufuata sheria 17 za soka

"Sisi tuko kamili, maandalizi tumefanya ya kutosha na timu yetu sasa iko vizuri. Tunasema hivi, Jumapili tutaupiga mpira mwingi tu mashabiki wetu waje kwa wingi wapate burudani. Nawahakikishia bila ya makandokando hatuwezi kufungwa.."

"Makandokando ninayozungumzia ni kama matukio yaliyotokea katika mchezo waliocheza na Azam Fc juzi. Kama masuala kama yale hayatakuwepo, hawawezi kutufunga," alitamba Nugaz

Mhamasishaji huyo wa Yanga amewataka mashabiki kuchangamkia ofa ya punguzo la mauzo ya jezi za Yanga ili Jumapili wapendeze na uzi wa Yanga

"Jezi zinapatikana kwa Tsh 20,000/- tu kwenye maduka yote ya GSM pamoja na Mawakala. Lakini pia unaweza kufika Makao Makuu ya klabu ya Yanga kujipatia jezi pamoja na tiketi kwa ajili ya mchezo huo"

Post a Comment

0 Comments