BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU 11-11-2019

Manchester United inaweza kushawishika kujaribu kumrejesha tena mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic katika Old Trafford.
Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 38- -mchezaji wa kimataifa wa Sweden atakuwa huru kutokana na kwamba mkataba wake na klabu ya ligi ya MLS - LA Galaxy unakaribia kumalizika.
(TuttoMercatoWeb, via Mail)
Uongozi wa Arsenal uko nyuma kwa "100%" ya meneja Unai Emery na mpango wa kusubiri hadi ufike msimu mwingine kabla ya kufanya maamuzi kuhusu hali ya baadae ya Muhispani huyo. (Athletic - subscription required)
Meneja wa zamani wa Spain Luis Enrique, ambaye amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwa meneja mbadala atakayechukua nafasi ya Emery katika klabu ya Arsenal, hatafikiria kurejea kwenye utawala kwa sasa . (ESPN)
Tottenham watamuhamisha winga wa Ajax na Morocco, Hakim Ziyech, mwenye umri wa miaka 26, wakati ambao Mchezaji wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, ataondoka katika klabu hiyo. (90min)
Baba yake mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar anasema kuwa hatafanya mazungumzo na Barcelona juu ya kurejea kwa mwanae katika klabu ya Nou Camp na kwamba mchezaji huyo wa safu ya mashambulizi mwenye umri wa miaka 27 atabaki katika klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain. (ESPN Brazil, via Mail)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, mwenye umri wa miaka 28, amekana taarifa zinanazomuhusisha na kuhamia katika klabu ya Real Madrid na anasema kuwa anaweza kumalizia taaluma yake ya soka katika Stamford Bridge. (Sun)
Burnley wamekamilisha mipango ya kumaliza mkopo wa kiungo wa kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 29 Dann Danny Drinkwater katika klabu hiyo ifikapo mwezi Januari. (Sun)

Post a Comment

0 Comments