advertise with us

ADVERTISE HERE

HII HAPA HISTORIA YA KOCHA MPYA WA YANGA

napozungumzia magwiji wa soka la Tanzania utaonekana wa ajabu endapo utaliweka kando jina la Charles Boniface Mkwasa. Boniface Mkwasa alizaliwa tarehe 10 April 1955 



mkoani Morogoro alipopata elimu yake ya msingi na sekondari toka akiwa shule ya msingi na baadae sekondari alionesha uwezo mkubwa wa kucheza soka eneo la kiungo.

Mkwasa anakumbukwa sana na wakazi wa Morogoro akiwika na kikosi cha Mseto toka mwaka 1973 mpaka 75 akisimama kama beki wa kati na kiungo mkabaji aliiwezesha timu hiyo kuibuka mabingwa wa ligi daraja la kwanza mwaka 1975 ikiwa timu ya kwanza kuchukua kombe hilo nje ya Dar es salaam.

Mkwasa aliihama Mseto mwala 1976 na kuamia Tumbaku hapo hapo mkoani Morogoro timu aliyoichezea hadi mwaka 1979 alipojiunga na timu yake kipenzi Yanga SC aliyoichezea bila kuhama mpaka anastaafu mpira mpira wake kiungo huyu mahili kuwahi kutokea nchini .

Mkwasa aliweza kuichezea Yanga SC kwa miaka kumi mfululizo mpaka alipostaafu mwaka 1989 . Rekodi inayomfanya kuingia kwenye orodha ya magwiji wa klabu hiyo waliyoichezea klabu hiyo bila kuhama.

Kitaaluma
Mwalimu Mkwasa alianza mafunzo yake ya ukocha hapa nchini mwaka 1988 mwaka mmoja kabla hajastaafu soka . Uwezo mzuri ulimpa fursa kwenda nchini Brazil mwaka 1991 kuchukua diploma ya taaluma hiyo . Alionesha uwezo mzuri darasani na mafunzo kwa vitendo na aliporudi nchini alirejea kwenye klabu yake kama kocha msaidizi chini ya hayati Syllersaid Mzirayi.

Mwaka 2000 alipata fursa tena ya kwenda Ujerumani alipopata diploma nyingine ya ukocha na kupata leseni ya daraja A .

Sio wana Yanga SC wanaofurahia matunda ya mwalimu huyu bali pia Tanzania Prisons mwaka 1999 akiwa kocha mkuu aliiwezesha kuibuka mabingwa wa ligi ya Muungano ambayo kwa sasa haipo.

Mwaka 2001 alikuwa Msaidizi wa Mziray chini ya Mshauri wa Ufundi, Mjerumani Burkhad Pape katika kikosi Taifa Stars kilichotwaa ubingwa wa Kombe la mataifa manne, Castle Cup.

Mwaka 2002, yeye na Mziray waliifiksiha timu ya Bara fainali ya Kombe la Challenge na mwaka 2007 akapewa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kama Kocha Mkuu, lakini haikufanya vizuri baada ya kuambulia nafasi ya nne.


WASIFU WA CHARLES BONIFACE MKWASA;
KUZALIWA: 10 Aprili 1955 (Miaka 60)
ALIPOZALIWA: Morogoro, Tanzania
NAFASI: Beki/Kiungo
TIMU: Tanzania 
KLABU ALIZOCHEZEA:
Mwaka                      Timu                                      
1973–1975               Mseto FC
1976–1978               Tumbaku                  
1979–1989               Yanga SC
ELIMU YA UKOCHA
1988: Kozi ya Awali
1989: Kozi ya Kati
1989: Kozi ya Juu
1991: Diploma (Brazil)
2000: Diploma (Ujerumani)
HADHI ZA KITAALUMA;
Ana leseni A ya CAF (Tangu 2014)
Ni Mkufunzi wa CAF (tangu 2014)
TIMU ALIZOFUNDISHA
1989–1991   Super Stars   (Kocha Mkuu)
1991–1993   Yanga SC       (Msaidizi wa Syllersaid Mziray)
1994–1996   Sigara            (Kocha Mkuu)
1998-1999    Al Khaboura (Oman, Kocha Mkuu)
1999-2000    Tanzania Prisons
2001-2002    Yanga SC
2002               Coastal Union
2003               Tanzania Prisons
2005               Moro United
2006               Miembeni
2008               African Lyon
2008-2013     Ruvu Shooting
2013-2014     Al Shoolai (Saudi Arabia)
2014:              Yanga SC
TIMU ZA TAIFA
1992-1993: Tanzania Bara B ‘Kakakuona’ (Msaidizi wa Sunday Kayuni)
1993-1994; Tanzania timu ya vijana U17 (Kocha Mkuu)
2001-2003: Tanzania Bara (Msaidizi wa Syllersaid Mziray)
2007-2008: Tanzania Bara (Kocha Mkuu)
2008-2013; Timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’, (Kocha Mkuu)
2015-          Tanzania 'Taifa Stars' (Kocha Mkuu)
MATAJI TUZO:
WAKATI ANACHEZA; Ubingwa wa Ligi Kuu Bara; 1975 (Mseto), 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, (Yanga SC).
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati; 1986 (Washindi wa Pili)
TUZO BINAFSI;
1975: Mchezaji Bora chipukizi Tanzania
1981: Mchezaji Bora Tanzania
AKIWA KOCHA; 
Ligi Kuu Bara; Ubingwa 1991, 1992, 1993, 2015 (Yanga SC)
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati; Ubingwa 1993 (Kampala, Uganda)
Ngao ya Jamii; Ushindi 2001 na 2014 (Yanga SC)
Kocha Bora Tanzania; 1999 na 2005
TIMU ZA TAIFA;
Ubingwa Kombe la Castle; 2001  (Taifa Stars)
Tiketi ya Fainali za AFCON; 2010 (Twiga Stars)
Washindi wa tatu COSAFA; 2011 (Twiga Stars)
Tiketi ya Michezo ya Afrika; 2011 (Twiga Stars)

Post a Comment

0 Comments