BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YATINGA TFF KUDAI ALAMA TATU

 Yanga Princess imepeleka malalamiko Shirikisho la Soka (TFF) baada ya kugundua Alliance Girls imemtumia mchezaji wa kigeni kinyume na sheria.Oktoba 12 Uwanja wa Nyamagana zilikutana timu hizo kwenye mchezo wa raundi ya pili ya wanawake na mechi ikitamatika wa sare ya bila kufungana.



Baada ya Yanga kugundua kuwa timu hiyo ilifanya udanganyifu kwa kumtumia mchezaji huyo ilipeleka malalamiko kwa TFF.

Alipotafutwa Mratibu wa Yanga, Kibwana Matokeo juu ya sakata hilo alisema, “ni kweli tumepeleka malalamiko.” Huku akikataa kufafanua jambo hilo.

Kwa upande wake Mwenyeiti wa Akademi ya Alliance, Nyaitati Stephano alisema hawajapokea barua yoyote kutoka TFF.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania (TWFA), Somoe Ng’itu alisema kama kamati wameyapokea malalamiko hayo na watakutana kutolea uamuzi.

Kama itathibitishwa Alliance ilimchezesha mchezaji huyo itapokonywa pointi tatu na faini ya Sh500,000 akitozwa mchezaji, kwa mujibu wa kanuni.

Hii sio mara ya kwanza kwa Alliance kumchezesha mchezaji kwani msimu uliopita ilimtumia Nelly Kache ambaye hakuwa na uhalali na mechi hiyo baada ya kuwa na kadi tatu kwenye mechi dhidi ya Geita Queens na kupokonywa pointi tatu.

Post a Comment

0 Comments