Bao la Moises Caicedo liliinyima Manchester United ushindi katika mechi yao ya kwanza ya Premier League tangu kumtimua Erik ten Hag huku Chelsea ikiambulia sare ya 1-1 Old Trafford.
Bosi wa muda Ruud van Nistelrooy, ambaye nafasi yake itachukuliwa na Ruben Amorim,Kocha huyo alijawa na furaha baada ya Bruno Fernandes kuiweka United mbele kwa mkwaju wa penalti dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika lakini Caicedo alisawazisha bao hilo kwa haraka na kurejesha matumaini kwa The Blues ambao walikua juu ya Arsenal kwa tofauti ya mabao manne. Sare hii ya Chelsea inawafanya kufikisha alama 18 katika michezo 10 waliyocheza wakisalia nafasi ya 4 juu ya Arsenal na Ason Villa wenye alama 18
Pointi moja inaiacha United ikiwa bado chini katika nafasi ya 13, pointi sita kutoka kwenye nafasi nne za juu. Amorim hakuhudhuria mchezo huo akijiandaa kukabidhi mikoba ya Sporting Lisbon kwa mchezo mmoja wa Ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Manchester City siku ya Jumanne.
Kwa upande wa Van Nistelrooy huo ulikuwa mchezo wake wa pili bila kupoteza baada ya kupata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Leicester mchezo wa Carabao Cup na kufanikiwa kutinga hatua za robo fainali.
Kocha huyo wa mpito bado ni shujaa miongoni mwa mashabiki wa United tangu enzi zake akiwa mshambuliaji mahiri, jina la Mholanzi huyo liliimbwa katika mazingira mazuri ya kabla ya mechi. Hata hivyo, timu ya Chelsea ambayo imepoteza mara moja katika mechi tisa za Ligi Kuu ya Uingereza, ilitoa mtihani mgumu zaidi kwa timu ya United ambayo bado haijajiamini. Noni Madueke alikaribia kuifungia Chelsea bao la kwanza katika kipindi cha kwanza alipounganisha kwa kichwa kona ya Cole Palmer .
Ujio wa Amorim utawafanya United kuongozwa na kocha wa pili kutoka Ureno baada ya Jose Mourinho kutwaa mataji mawili akiwa na kikosi hicho. Wengi wanaamini Amorim ni chaguo sahihi kwa United kwa sababu ya uwezo wake wa kushinda makombe alipokuwa ureno akifanya hivyo mara 5 lakini umri wake wa miaka 39 utatengeneza mahusiano mazuri baina yake na wachezaji wa kigeni.
0 Comments