Ligi ya mabingwa ulaya inaendelea leo jioni kwa mechi 9 kuchezwa barani humo.Hii ni raundi ya nne kwa timu zote shiriki na michezo hiyo itachezwa viwanja mbalimbali kwa nyakati tofauti. Michezo ya awali itawakutanisha Slovan Bratislava dhidi ya Dinamo Zagreb pamoja na PSV dhidi ya Girona.Michezo hiyo itapigwa majira ya saa 8:45 Usiku wa leo ikifuatiwa na michezo mingine ya saa 5 usiku.
Mchezo uliobeba hisia za wengi ni ule unaowakutanisha Real Madrid dhidi ya AC Milan timu zenye historia kubwa kwenye michuano hiyo.Real Madrid ndiye bingwa mtetezi wa michuano hiyo akiwa na rekodi ya kutwaa mataji 15 akifuatiwa na AC Milan wenye mataji 7 .
Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana katika michuano hiyo ni msimu wa 2010/11 mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2. Mpaka sasa timu hizo zimecheza michezo 15 na zote zikishinda michezo 6 kwa kila mmoja na sare 3.Timu hizo zimefungana jumla ya mabao 49.Real Madrid wakifunga mabao 25 na Ac Milan wakifunga mabao 24
Hii hapa ratiba ya michezo itakayopigwa siku ya le0
0 Comments