BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA USAJILI DUNIANI NOVEMBA 5

 Inter Milan na Barcelona wanamuwania Enzo Fernandez wa Chelsea, Alexander Isak wa Newcastle analengwa na Arsenal na Manchester United wanakabiliwa na ushindani katika kinyang’anyiro cha kumnunua Geovany Quenda wa Sporting.

Inter Milan na Barcelona wanapanga kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Argentina Enzo Fernandez, 23, ambaye mustakabali wake Stamford Bridge haujabainika. (Sun)

Arsenal wamemtambua mshambuliaji wa Newcastle Alexander Isak, 25, kama lengo lao kuu la uhamisho, ingawa Magpies wanadai ada ya takriban pauni milioni 100 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswidi. (Team Talk)



Manchester United wanamtaka winga wa Sporting Geovany Quenda, 17, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno chini ya miaka 21 pia akilengwa na Manchester City, Liverpool na Juventus. (Team Talk)

Kocha wa Manchester United aliyetimuliwa Erik ten Hag hakutaka kumnunua mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee kutoka Bologna msimu wa joto na alikasirika wakati ulipowasili kwa ajili ya kufanya mazoezi. (Sun)

Tottenham wanavutiwa na kiungo wa kati wa Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, lakini hawana uwezo wa kumnunua kutoka AC Milan mwezi Januari. (Football Insider)

Chelsea hawana nia ya kumuuza mlinzi Benoit Badiashile, 23, huku beki huyo wa Ufaransa akizingatiwa kuwa sehemu ya mipango yao ya muda mrefu. (Fabrizio Romano)

Nottingham Forest ingependa kumchukua winga wa Bayern Munich Mathys Tel, 19, kwa mkopo lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa wa chini ya miaka 21 hana mpango wa kuondoka Bavaria msimu huu wa baridi. (Sky Germany)

Kocha wa zamani wa Chelsea na Everton, Frank Lampard, ameibuka kama mgombea anayepigiwa upatu kuchukua mikoba ya mkufunzi Ivan Juric anayekabiliwa na shinikizo ikiwa Roma itaamua kumfuta raia huyo wa Croatia. (Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano)

Tottenham watazingatia chaguo la mwaka mmoja kwenye kandarasi ya mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min, 32. (Telegraph – usajili unahitajika)

Son

Chanzo cha picha,Getty Images

Manchester United itampa kocha mpya Ruben Amorim usemi kabla ya kufanya maamuzi ya kandarasi kuhusu wachezaji wanaokaribia mwisho wa mikataba yao. (ESPN)

Aston Villa wanakaribia kuafikiana kandarasi mpya na mshambulizi Muingereza Morgan Rogers, 22. (Football Insider)

Edu anatazamiwa kuchukua jukumu la mtandao wa vilabu vinavyodhibitiwa na mmiliki wa Nottingham Forest Evangelos Marinakis baada ya kujiuzulu kama mkurugenzi wa michezo wa Arsenal. (Times- usajili unahitajika)

Post a Comment

0 Comments