BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA USAJILI DUNIANI NOVEMBA 4

 Trent Alexander-Arnold yuko kwenye orodha ya beki wanaosakwa na Real Madrid, Newcastle wanamtaka Bryan Mbeumo, Arsenal wanajiandaa kumnunua Mohammed Kudus.Real Madrid wanavutiwa sana na beki wa Liverpool na Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, wanapojiandaa kuimarisha safu yao ya ulinzi. (AS - kwa Kihispania)



Newcastle United wamemjumuisha winga wa Cameroon Bryan Mbeumo kwenye orodha ya wachezaji wanaowataka, huku Brentford ikiweka bei ya pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)

Arsenal wanataka kumnunua winga wa West Ham wa Ghana Mohammed Kudus, 24, kama mbadala wa mshambuliaji wa Ubelgiji Leandro Trossard, 29, ambaye anawaniwa na klabu ya Al-Ittihad ya Saudia. (Mirror)

Mshambuliaji wa Reims kutoka Ivory Coast Oumar Diakite, 20, atakuwa kipaumbele cha Crystal Palace ikiwa mazungumzo ya kandarasi kati yao na mshambuliaji wao Mfaransa Jean-Philippe Mateta, 27 yatagonga mwamba. (Sun)

Manchester United na Chelsea wameungana na Tottenham katika mbio za kumsajili beki wa Denmark Patrick Dorgu, 20, kutoka Lecce. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Uingereza Lewis O'Brien, 26, anatarajiwa kuhamia Los Angeles FC kwa dau la pauni milioni 7 wakati mkopo wake kutoka Nottingham Forest utakapokamilika Januari. (Sun)

Kocha wa West Ham Julen Lopetegui anakabiliwa na shinikizo kubwa la kuondoka mapema baada ya kuufahamishwa na klabu kwamba matokeo lazima yaboreshwe. (Times - usajili unahitajika)

Paris St-Germain na Randal Kolo Muani wako tayari kwa uhamisho wa mkopo wa mwezi Januari mwakani, wakiwa na chaguo la kununua, na baadhi ya vilabu vya Ligi ya Premia tayari vimewasilisha maombi ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 25. (Sky Sport Germany)

Barcelona wanafuatilia hali ya Rafael Leao katika klabu ya AC Milan iwapo winga huyo wa Ureno, 25, atapatikana. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

xx

Chanzo cha picha,Getty Images

Real Madrid wameanza kutilia shaka dhamira ya Vinicius Jr katika klabu hiyo na wana wasiwasi kuwa atafikiria kuondoka, huku Al-Hilal wakiwa na nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Brazil, 24. (Sport - kwa Kihispania), kutoka nje.

Chelsea na Paris St-Germain pia wanavutiwa na Vinicius Jr na maafisa wa Real Madrid watakutana na wawakilishi wake baada ya wiki chache kujadili mustakabali wake. (Marca - kwa Kihispania), nje

Santos iko kwenye mazungumzo ya kumrejesha Neymar katika klabu hiyo wakati mkataba wake na Al-Hilal utakapokamilika msimu ujao. Mshambuliaji huyo wa Brazil, 32, alikatiza mkutano na wanahabari kwa njia ya video baada ya mechi. (AS - kwa Kihispania)

Lazio ni miongoni mwa klabu zinazowania kumsajili James Rodriguez iwapo winga huyo wa Colombia, 33, atamaliza jukumu lake Rayo Vallecano. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Post a Comment

0 Comments