Mkufunzi wa Liverpool Arne Slot yuko tayari kuwauza makipa Alisson Becker na Caoimhin Kelleher, Chelsea hawana nia ya kumnunua Kelleher, na Arsenal wamemteua Alexander Isak kuwa mlengwa wao mkuu wa uhamisho.
Kocha wa Liverpool Arne Slot yuko tayari kumuuza mlinda lango wa Brazil Alisson Becker, 31, na wa Ireland Kaskazini Caoimhin Kelleher, 25, msimu ujao wakati mchezaji wa Valencia na Georgia Giorgi Mamadashvili, 24, atakapojiunga na klabu hiyo. (TBR)
Chelsea haitamnunua Kelleher kwani kocha mkuu Enzo Maresca ameridhika na chaguo zake za sasa. (Give Me Sport)
Arsenal wamemfanya mshambuliaji wa Newcastle na Uswidi Alexander Isak, 25, kuwa kipaumbele chao ushambuliaji, huku Magpies wakipmsaka Muingereza Dominic Calvert-Lewin, 27, wa Everton na Jonathan David, 24, wa Lille na Canada kama mbadala. (TeamTalk)
The Gunners pia wana nia ya kumnunua winga wa Real Madrid na Uturuki Arda Guler mwenye umri wa miaka 19. (Sport – kwa Kihispania)
Liverpool wamefufua mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Ufaransa Marcus Thuram, 27, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 70 ambacho kitaanza kutumika hadi mwisho wa msimu wa 2027-28. (Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano)
Liverpool wanamtaka winga wa Misri na klabu ya Eintracht Frankfurt Omar Marmoush, 25, kama mbadala wa Mohamed Salah. (Give me Sport)
Kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso, 42, ambaye anawaniwa na klabu kama kama Real Madrid, atafanya uamuzi kuhusu hatma yake mwezi Machi. (Marca kwa Kihispania)
Agenti wa mchezaji wa Tottenham Hotspur Radu Dragusin, 22, imefuta uwezekano wa uhamisho wa mkopo wa beki huyo wa Romania mwezi Januari, lakini amedokeza kuhusu uhamisho wa majira ya joto. (Tuttomercato – kwa Kiitaliano)
Galatasaray wana nia ya kumsajili nahodha wa Tottenham Hotspur na Korea Kusini Son Heung-min, 32, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Ligi ya Premia unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Fanatic – kwa Kituruki)
Kipaumbele cha Aston Villa dirisha la usajili wa wachezaji litakapofunguliwa mwezi Januari kitakuwa kupata beki mpya, huku kiungo wa Real Betis Mhispania Diego Llorente, 31, akiwa kwenye orodha yao fupi. (Football Insider)
Manchester City wanatathmini uwezekano wa kumnunua mlinzi wa RB Leipzig na Ufaransa Castello Lukeba, 21, huku wakijiandaa kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Football transfers)
Newcastle wanatazamia kumnunua winga wa Sporting na Ureno Geovany Quenda, 17, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester United na Chelsea. (Give Me Sport)
Arsenal wanafikiria kumnunua kiungo wa Southampton na Ireland Kaskazini Shea Charles, 21, ambaye amefanya vyema katika klabu ya Sheffield Wednesday. (Fichajes – kwa Kihispania)
Southampton wamedokeza nia ya kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil Endrck, 18, pamoja na Roma na Real Valladolid. (Sport via Mirror),
Crystal Palace itamsajili mshambuliaji mpya katika dirisha la usajili la Januari, fedha zikipatikana baada ya kuondoka kwa Michael Olise na Joachim Andersen majira ya kiangazi. (Football Insider)
Lyon wanataka pauni milioni 25 kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa Rayan Cherki, 21, huku Liverpool na Bayer Leverkusen zikiwa miongoni mwa klabu zinazomuwania. (Footmercato)
Barcelona ilikataa dau la euro milioni 250 kutoka kwa Paris St-Germain kwa ajili ya winga wa Uhispania Lamine Yamal, 17, msimu uliopita (El Chiringuito via 90min)
PSG wamekanusha kuwasilisha ombi hilo, wakisema hawakuwa katika nafasi ya kutumia kiasi hicho cha fedha msimu uliopita. (L’Equipe)
0 Comments