Erling Haaland yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa pesa nyingi na Manchester City, West Ham wanamtaka kiungo wa City James McAtee, Aston Villa wanataka kumsajili beki wa kati wa Uhispania Diego Llorente.
Manchester City wanazidi kuamini kuwa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 24, atasaini mkataba mpya katika klabu hiyo ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi katika Ligi ya Premia. (Mirror)
West Ham wanatazamia kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City Muingereza James McAtee, 22, huku wakihofia kumpoteza fowadi wa Brazil Lucas Paqueta, 27, mwezi Januari.(Sun)
Ruud van Nistelrooy analenga kibarua cha Premier League baada ya kusikitishwa na kuondoka kwake Manchester United. (Mirror)
Mustakabali wa meneja wa Luton Rob Edwards katika klabu hiyo uko mashakani huku Coventry ikitazama matukio yanavyofanyika.(Sun)
Meneja wa Aston Villa Unai Emery anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili mlinzi wa kati wa Uhispania Diego Llorente, 31, kutoka Real Betis Januari lakini mkataba wa muda mrefu wa beki huyo unaweza kuwa kikwazo. (Football Insider)
Aston Villa pia wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo mshambuliaji wa Athletic Bilbao Mhispania Oihan Sancet, 24, lakini hawana uhakika kama watatimiza masharti yake ya euro 80m (£66.9m)(Caught Offside)
Juventus wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Uholanzi Joshua Zirkzee, 23, huku mustakabali wa fowadi wao Mserbia Dusan Vlahovic, 24, ukiwa katika mizani. (CalcioMercato - kwa Kiitaliano)
Mshambulizi wa Nigeria Victor Osimhen, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray , atapatikana kwa euro 75m (£62.7m) msimu wa joto, kulingana na kifungu cha kuachiliwa kilichowekwa katika mkataba wa hivi punde zaidi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 na Napoli . (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Newcastle inaweza kulenga kumuuza mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, na kutumia pesa hizokumnunua mbadala wa kiwango cha kimataifa. (Football Insider)
Beki wa kati wa Ujerumani Jonathan Tah, 28, hatatia saini mkataba mpya na mabingwa wa Bundesliga Bayer Leverkusen na kuhamia Bayern Munich au Barcelona kwa uhamisho wa bila malipo ni "chaguo halisi". (Sky Sports Ujerumani)
Beki wa Paris St-Germain Milan Skriniar , 29, yuko tayari kurejea Italia na Juventus huku Mslovakia huyo akiendelea kutatizika kupata muda wa kucheza katika klabu hiyo ya Ufaransa. (La Gazzetta dello Sport,- kwa Kiitaliano )
0 Comments