BETI NASI UTAJIRIKE

STARS NJIA NYEUPE KUFUZU AFCON 2025

 Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia umeendelea kuiweka Taifa Stars katika mbio za kuwania kushiriki michuano ya AFCON 2025 inayokwenda kupigwa nchini Morocco.Ushindi huo unaifanya Taifa stars kushika nafasi ya tatu ikiwa na alama 7 katika michezo 5 iliyocheza wakigombea nafasi hiyo na Guinea yenye alama 9 katika michezo 5.



Stars itapanda dimbani siku ya Novemba 19 dhidi ya Guinea katika Dimba la Benjamini Mkapa na kama itaibuka na ushindi basi itafuzu moja kwa moja kushiriki michuano hiyo muhimu kwa taifa letu.

Tathmini ya mchezo dhidi ya Ethiopia

Taifa Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia mchezo uliopigwa nchini DRC.Simon Msuva alianza kuifungia Taifa Stars dakika ya 15 akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Novatus Miroshi.

Tanzania iliendelea kutawala mchezo, na kujinufaisha maradufu katika dakika ya 31 Feisal Salum alipounganisha kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Ethiopia walitatizika kupata nafasi za kufunga katika muda wote wa mechi, huku nafasi zao bora zikipatikana mwishoni mwa kipindi cha pili.Birhanu Bekele na Abdulkerim Worku wote walimjaribu kipa wa Tanzania Aishi Manula lakini hawakuweza kuufumania nyavu.

Ushindi huo unaifanya Tanzania kushika nafasi ya tatu katika Kundi H ikiwa na pointi saba, nyuma ya Guinea kwa alama 2. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikiwa tayari imefuzu, pambano la kuwania tiketi ya pili ya kundi hilo kwa TotalEnergies CAF AFCON bado liko wazi, na kuongeza fitina zaidi katika awamu ya mwisho ya mechi za kundi hilo.

Ethiopia, ambayo imejikita mkiani mwa kundi hilo ikiwa na pointi moja pekee, imeondolewa kwenye michuano. Licha ya kujaribu kwa bidii, Walia Ibex hawakuweza kuvunja msururu wao wa kutoshinda katika mchujo huo.

Ikiwa imesalia na mechi moja ya mchujo, Taifa Stars sasa iko katika nafasi nzuri ya kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano hiyo.Katika mchezo huo  Kocha Hemed Suleiman Mmorocco alianza na Aishi Manula,Shomari Kapombe ,Mohammed Husein Ibrahim Hamad 'Bacca',Dickson Job ,Miroshi,Mudathir Yahya ,Msuva ,Feisal Salum,Clement Mzize na Mbwana Samatta.

Stars walikuwa bora zaidi eneo la ushambuliaji wakipiga mashuti 20 na kati ya hayo 7 yalikwenda langoni huku mengine 13 yakikosa muelekeo.

Post a Comment

0 Comments