Ligi ya Soka ya Samia Cup mkoa wa Kagera imeendelea hapo jana kwa hatua ya nusu fainali ya kwanza ikiwakutanisha Karagwe FC dhidi ya Bukoba Manispaa katika dimba la Mashujaa Bunazi wilayani Missenyi mkoani Kagera.Lengo kuu la michuano hiyo ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27.
Tathmini ya mchezo
Bukoba Manispaa walikuwa wa kwanza kupata bao la uongozi likiwekwa kimiani na kiungo mshambuliaji Ramadhani Kapilima dakika ya 39 lakini bao hilo lilidumu kwa dakika moja tu ambapo Isaac Kachwele aliisawazishia Karagwe FC. Mchezo huo ulikwenda mapumziko kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa mabao 1-1.
Dakika ya 62 Isaac Kachwele alirejea langoni mwa Bukoba Manispaa na kupachika bao la pili lililodumu mpaka dakika ya 90. Ushindi wa mabao 2-1 unawafanya Karagwe kuingia fainali za michuano hiyo.
Leogiger Kachebinao apongezwa
Mgeni Rasmi katika mchezo huo Bw. Faris Buruhan ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm Mkoa Kagera amempongeza kijana aliyeanzisha ligi hiyo Ndg.Leodiger Kachebinao ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya KPD wakishirikiana na Shadafa pamoja na Clouds Media kwa uzalendo waliouonyesha wakiwa na lengo zuri la kuimarisha umoja na mshikamano kwa jamii.
“Tumeona michezo ni ajira kama ambavyo tutaona mshindi wa kwanza wa pili na watatu wakipata kipato kutokana na michezo hii ,wito wangu ni kuendeleza mshikamano huu ifikapo tarehe 27 novemba mwaka huu kupiga kura kwa viongozi bora wenye sifa kuwaletea maendeleo kwenye vijiji na vitongoji” amesema Mwenyekiti Buruhan.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashari kuu ccm taifa kutoka mkoa wa Kagera (Mnec) Karim Amry ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi wasipuuzie uchaguzi huo
0 Comments