BETI NASI UTAJIRIKE

PSG: UFALME WA MBAPPE UMECHUKULIWA NA NYOTA HAWA

 PSG imeendeleza ubabe wake Ligue 1 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lens.Ushindi huo unawafanya PSG kufikisha alama 26 katika michezo 10 waliyocheza. Timu hiyo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa ikiibuka na ushindi michezo 8 na sare 2.


Bao la Osuman Dembele liliwafanya PSG kujihakikishia uongozi wa ligi kwa tofauti ya alama 6 dhidi ya wapinzani wao Marseille Olympic pamoja na Monaco wanashika nafasi ya pili na tatu wakiwa na alama 20 kila mmoja na kutofautiana kwa mabao ya kufunga.

Mashabiki wa PSG ni kama wamesahau uwepo wa Kylian Mbappe aliyeondoka klabuni hapo kama mchezaji huru na kutua Real Madrid ,Kwa sasa wameweka mategemeo yao kwa Mfaransa mwenzake Bradley Barcola aliyefunga mabao 8 na kutengeneza mabao 2 katika michezo 10 aliyocheza Ligue 1 msimu huu.

Tegemeo la pili wameweka kwa Mfaransa mwingine ambaye ni Ousmane Dembele aliyefunga mabao 5 na kutengeneza mengine  4 katika mechi 9 alizocheza mpaka sasa. Nyota hao wamekuwa nguzo muhimu kwa PSG msimu huu na mashabiki wanawapa heshima yao

Post a Comment

0 Comments