BETI NASI UTAJIRIKE

PAMBA JIJI YATUMA SALAMU,MDAU KUTOA MAMILIONI WAKIIBOMOA SIMBA

 Klabu ya Pamba jiji imeendelea na mazoezi makali kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Simba mchezo utakaopigwa dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza. Pamba jiji wanaonolewa na kocha Fredrick Minziro wameshinda mchezo mmoja pekee kati ya michezo 11 iliyocheza mpaka sasa.



Msimamo wa ligi unaonyesha Pamba jiji wakishika nafasi ya 15 kati ya timu 16 wakiwa na alama 8 pekee.Timu hiyo inaongoza kwa kufungwa michezo mingi ikiwa imefungwa michezo 5 na sare 5.Wapinzani wao Simba SC wanaongoza ligi wakiwa na alama 25 katika michezo 10 waliyocheza wakipoteza mchezo 1 na sare 1 pekee.

Pamba jiji wako wapi

Taarifa zisizo rasmi zimeeleza kwamba klabu hiyo imeweka kambi mkoani Shinyanga kujiandaa na mchezo huo muhimu. Kikosi cha Minziro kinaamini kama watapata ushindi katika mchezo huo basi watarejesha imani kwa mashabiki na viongozi wake huku morali ikipanda kwa wachezaji kufanya vyema.

Wajuzi wa mambo wanasema donge la milioni 40 litatolewa na mdau wa soka endapo wataibuka na ushindi katika mchezo huo na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.Mtanda amenuliwa akisema

‘Pamba jiji kesho tunacheza na Simba na matarajio yetu  ni kuwafunga Simba,sasa wengine hawaamini ila mimi nawaambia kwa uwezo wa Mungu Simba inaenda kufungwa na Pamba lakini kama hawaamini waende wakaangalie namna ambavyo Yanga alifungwa na Tabora 

Post a Comment

0 Comments